Uhalisia katika mashairi ya Kezilahabi (Dhifa)
Abstract
Fasihi ni kioo cha maisha. Humulika jinsi jamii ilivyo kwa kuangazia masuala mbalimbali yanayoikumba. Waandishi wa kazi za fasihi huchota maudhui yao kutokana na matukio mbalimbali yanayoikumba jamii, nia yao ikiwa ni kuielimisha, kuiadilisha na kubeza maovu yanayotendeka. Makala hii inaangazia uhalisia katika mashairi ya Diwani ya Dhifa iliyoandikwa na Euphrase Kezilahabi (2008). Kupitia kwa mashairi yake, Kezilahabi ameichora hali halisi iliyopo katika mataifa mengi ya Afrika kwa kumulika matatizo mbalimbali yanayoyakumba. Anaupitisha ujumbe wake kwa kutoa taswira nzito zinazoundwa kutokana na matumizi ya tamathali mbalimbali za usemi ambazo zinaacha athari kubwa kwa wasomaji na kuwachochea kupata ari ya kupigania haki za wanyoge. Utafiti huu unaongozwa na nadharia ya uhalisia, ambayo kulingana na Wamitila 2002, iliwekewa msingi na mwanafalsafa Hegel katika kitabu chake kinachojulikana kama Aesthetik. Utafiti unawawezesha wanajamii hasa kutoka mataifa ya Kiafrika kuyabaini matatizo mbalimbali wanayokumbana nayo na jinsi ya kujinasua kutokana na minyororo ya umaskini.
URI
https://www.researchgate.net/publication/364542260_Uhalisia_katika_mashairi_ya_Kezilahabi_Dhifahttps://doi.org/10.51317/eajk.v4i1.183
http://repository.mut.ac.ke:8080/xmlui/handle/123456789/6422
https://journals.editononline.com/index.php/eajk/article/view/183