Uchunguzi wa Kiaktantia wa Matangazo ya Biashara ya Kampuni ya Safaricom
Abstract
Uchanganuzi wa matangazo ya biashara umefanywa kwa kina. Baadhi ya wataalamu wamechunguza lugha na ishara mbalimbali wakiongozwa na Nadharia za Kisemiotiki. Makala hii inachukua mkondo tofauti kwa kuchanganua matangazo ya biashara ya Kampuni ya Safaricom kwa kuongozwa na mtazamo wa aktantia ulioasisiwa na Algirdas Julien Greimas mnamo mwaka wa 1966. Mtazamo huo umetumiwa kuchanganua hadithi mbalimbali zinazohusisha usimulizi kwa nia ya kubainisha majukumu mbalimbali yanayotekelezwa na wahusika katika hadithi hizo. Watafiti walichambua video tatu za matangazo ya biashara ya Kampuni ya Safaricom zilizopakuliwa kutoka katika mtandao wa YouTube. Makala hii inadhihirisha kuwa matangazo ya Safaricom aina ya video hudhihirisha ngazi sita za kiaktantia zinazoelezwa na Greimas katika mtazamo wake. Utafiti huu unaongezea maarifa mapya katika uchambuzi wa matangazo ya biashara.